
ALIYEKUWA beki wa Simba, Pascal Wawa ambaye sasa anakipiga Timu ya Singida Big Stars amejichora tatoo kwa bei mbaya. Mwili wa Wawa umejaa tatoo kila upande kuanzia kwenye shingo yake hadi kwenye miguu.
Alipoulizwa ni gharama gani ambayo ametumia kwenye kuchora tatoo zake alisema ni nyingi kiasi ambacho hakumbuki kwa sasa.

“Hii tatoo yangu ya mkono wa kushoto nakumbuka nilitumia masaa manne kuichora na nililipa sh 1 milioni, hizi zingine sikumbuki sana kiukweli ila nazo nilitumia pesa.
“Mke wangu na mama wanapenda sana tatoo kwa hiyo ndio maana nikawa nachora lakini sasa nimeona zimekuwa nyingi mwilini mwangu na nimeamua kuacha.” Wawa kwa sasa yupo katika kikosi cha Singida na ameendelea kupewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza huku akiiwezesha timu hiyo kufuzu kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.