The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Polisi Latembelea Ofisi za Vodacom Kukagua Usalama Sehemu za Kazi

0
Mkurugenzi Mendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire (kushoto) akipokea cheti cha ukaguzi wa gari pamoja na stika ya usalama barabarani kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Michael Deleli (kulia) wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam kujifunza namna inavyozingatia masuala ya afya na usalama mahala pa kazi. Ziara fupi ya uongozi wa Jeshi la Polisi la Tanzania ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi inayosherehekewa Aprili 28 ya kila mwaka. 

 

Jeshi la Polisi Tanzania, limefanya ziara kwenye ofisi za Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom kukagua usalama wa ofisi na magari yanayotumiwa na kampuni hiyo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi inayosherehekewa April 28, kila mwaka.

Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Michael Deleli akiwa Pamoja na Mkurugenzi Mendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, wakikagua injini ya mojawapo ya gari la kampuni hiyo walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam kujifunza namna inavyozingatia masuala ya afya na usalama mahala pa kazi. Ziara fupi ya uongozi wa Jeshi la Polisi la Tanzania ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi inayosherehekewa Aprili 28 ya kila mwaka.

 

Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Michael Deleli akiwa Pamoja na Mkurugenzi Mendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, wakikagua mojawapo ya gari la kampuni hiyo walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam kujifunza namna inavyozingatia masuala ya afya na usalama mahala pa kazi. Ziara fupi ya uongozi wa Jeshi la Polisi la Tanzania ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahala pa Kazi inayosherehekewa Aprili 28 ya kila mwaka.

 

 

Leave A Reply