×

Kocha Nabi Akiri Kikosi Chake Kuwa Na Matatizo Aongea Kiswahili “Kazi Bado” – Video

BENCHI la Ufundi la Yanga, limeweka wazi kuwa, lazima licheze michezo yote kwa ufasaha mkubwa na hawatategemea matokeo ambayo watayapata katika Uwanja wa Mkapa pekee dhidi ya Marumo Gallants.

Jana Jumatano, Yanga walikuwa na kibarua kizto cha kumenyana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika Mei 17, mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi, alisema: “Yanga tumejiandaa kuicheza michezo yote hii miwili, hatupo kwa ajili ya mchezo mmoja tu wa nyumbani kisha tuone kila kitu kimeishia, hapana.

“Nimewaambia wachezaji tayari tunatakiwa kupata matokeo mazuri katika kila uwanja ambao tunakwenda kucheza, kama sio nyumbani kwetu basi iwe hata ugenini, lazima tutambue huu ni mchezo mkubwa wa nusu fainali na tunatakiwa kucheza kikubwa.”

STORI NA MARCO MZUMBE

Leave a Comment