Tigo Wasaini Mkataba Mpya Awamu Ya 8 Kupeleka Mawasiliano Kata 371
Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imesaini mkataba mpya wa awamu ya 8 wa kufikisha huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini kwa ushiriikiano kati ya Tigo na Mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF). Kwa ujumla Tigo wanatarajiwa kujenga na kuboresha minara 409 katika kata 371 za vijijini hapa nchini.