Olamide akiwa na Don Jazzy.
SASA ni dhahiri kwamba ugomvi kati ya wanamuziki wawili wa Nigeria, Olamide na prodyuza wa kampuni ya Mavin, Don Jazzy, umezikwa na kusahaulika baada ya nyota hao kuamua kufanya kolabo.
Mwanamuziki w a kike, Tiwa Savage, ambaye ni First Lady wa kampuni ya Mavin na boss wa kampuni ya YBNL, Olamide, wamo katika matayarisho ya kufanya kolabo.
Habari hizo za kufurahisha zilitolewa na Don Jazzy kwenye ukurasa wake wa Instagram alipotoa picha ya Tiwa Savage na Olamide kutoka katika video ya singo yake mpya inayokwenda kwa jina la “Standing Ovation”.
Don alikuwa anatangaza video yake inayotarajiwa ambayo itatokana na albam ya Tiwa iitwayo RED! Yote kwa yote, jambo hilo limepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa pande mbili hizo.