The House of Favourite Newspapers

Fundi Ujenzi Amnyonga Mkewe Kisha Kujinyonga, Ndugu Wafunguka – Video

0

Fundi Ujenzi, Iddi Saidi Kindula (37), mkazi wa Madale jijini Dar es Salaam anadaiwa kumuua mkewe, Tukae Seif Ramadhani (16), kwa kumnyonga kisha naye kukutwa amefariki dunia akining’inia kwenye kamba chumbani kwao huku wakikiacha kichanga cha miezi minne kikiangua kilio muda mrefu bila msaada.

Tukae ambaye kwa sasa angekuwa kidato cha kwanza, ndugu zake wamesema alikataa shule kwa ajili ya kuolewa na mwanaume huyo asijue kama mapenzi hayo yangeweza kumbadilikia ndani ya kipindi kifupi akiwa na umri huo mdogo.

Kufuatia tukio hilo, mwanahabari wetu Richard Bukos alifika eneo la tukio na kuambiwa msiba wa mwanaume huyo umehamishiwa kwa ndugu zake na msiba wa Tukae umehamishiwa kwa wazazi wake ambapo mwanahabari wetu alielekezwa na kufika.

Akiwa msibani hapo, mwanahabari wetu aliwakuta ndugu waliojawa na huzuni wakiwa na kichanga kilichoachwa yatima na kifo cha kinyama kilichowakuta wazazi wake.

Mwanahabari wetu alizungumza na dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaidi Abdallah ambaye alinasimulia mkasa huo mwanzo mwisho.

Leave A Reply