Msanii wa Bongo Muvi na mjasiriamali anayemiliki mgahawa maarufu wa Shishi Food, Zuwena Mohamed @officialshilole amelamba dili la kuwa balozi wa vipodozi vya Safron.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhiwa ubalozi huo na mwanamama @estadalali_cosmetics ambaye ndiye msambazaji wa sabuni na cream za Safron akiwa na duka lake Sinza Madukani jijini Dar es Salaam, Shilole amenukuliwa akisema kwa kipindi kirefu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ngozi la utangotango lakini baada ya kuanza kutumia bidhaa hizo, tatizo hilo liliisha.