×

Wanahabari Wanolewa Kuripoti Habari Za Soko La Hisa

Mkurugenzi Mtendaji wa Soko la Hisa nchini, Miss Mary Mniwasa (kushoto) akifungua mafunzo hayo.

Dar es Salaam, 3 Juni 2023: Wanahabari nchini wamepata elimu ya uandishi wa habari za Soko la Hisa na kupata elimu ya ziada juu ya suala la uwekezaji wa hisa na faida zake kutoka Soko la Hisa Nchini, Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).

Akizungumza kwenye ufunguzi wa semina hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Soko la Hisa nchini, Miss Mary Mniwasa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwafanya wanahabari kuwa na uelewa juu ya uwekezaji wa hisa ili kuandika kiusahihi habari zinazohusiana na uwekezaji wa hisa.

Mkufunzi Ibrahim Mshindo akitoa mafunzo kwa wanahabari (hawapo pichani).

Katika semina hiyo wanahabari walijifunza namna ya kuwekeza kwa faida kwa kuzingatia vitu mbalimbali kama vile maadili ya soko, kiwango unachoruhusiwa kuwekeza, kipindi cha kizuri kuwekeza na mengineyo.

Katika mafunzo hayo wanahabari nao walitaka kujua nini kinatokea endapo taasisi uliyowekeza inapofilisika ambapo walijibiwa kuwa kwakuwa mwanahisa anakuwa miongoni mwa wamiliki na kuhusika mpaka kuchagua viongozi wa kampuni hivyo naye ni sehemu ya kampuni.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini kusikiliza.

Miongoni mwa wataalamu wabobezi wa masuala ya uwekezaji wa hisa waliotoa semina kwenye mafunzo hayo ni Mr. Emmanuel Nyalali, Ibrahim Mshindo na Lukas Sinkal ambapo kila mmoja alifundisha kipengele chake katika kutoa elimu hiyo.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.

Baada ya kupata mafunzo hayo wanahabari nao walishauriwa kuwekeza kwenye soko la hisa hili waweze kunufaika na faida inayopatikana na kuweza kuripoti vizuri habari hizo. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment