×

Simba Yawapora Yanga Kocha Wakubaliana Nae Kila Kitu

Mbrazil, Milton Nienov.

INAELEZWA kuwa, uongozi wa Simba umefikia makubaliano ya kumrudisha aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Mbrazil, Milton Nienov ambaye kwa sasa yupo Yanga akimaliza mkataba wake.

Taarifa zisizo na shaka zinadai kuwa, viongozi wa Simba wameshakubaliana kila kitu na kocha huyo, walikuwa wanasubiri jana Yanga wamalizane na Azam FC katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, ili kukamilisha jambo hilo.

“Ni kweli kuna maboresho makubwa ya benchi la ufundi kwa kuondolewa baadhi waliopo na kuletwa wapya kuja kuungana na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ambaye amewapendekeza kuja kufanya nao kazi,” alisema chanzo makini.

Ikumbukwe tayari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Gain’, alishaweka wazi juu ya suala la kuboresha benchi la ufundi la timu hiyo kwa kusema wanayajua makosa waliyofanya msimu huu, hivyo wamejipanga kufanya maboresho makubwa msimu ujao.

TUZO ya GOLI BORA na BEKI BORA ZAENDA YANGA, FISTON MAYELE na DICKSON JOB..

Leave a Comment