Mchungaji Anthony Lusekelo almaarufu Mzee wa Upako anasema kuwa mwanamke anapaswa kukaa nyumbani kwa ajili ya kulea watoto kwani anapotoka na mke naye anatoka mtoto kuna malezi anayakosa.
Ila hapingani na maendeleo ya sayansi na Teknolojia yanapaswa kuheshimiwa kwa mwanamke kufanya kazi ila kwa maoni yake anaona bora akae nyumbani.
Ameyasema hayo kupitia Kipindi cha Katikati ya Koko kinachorushwa na Global TV Online.