
Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya kilektroniki ya LG imefanya kweli tena baada ya kuwakutanisha mawakala katika semina iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LG Ukanda wa Afrika Mashariki, Dongwon Lee na ufanyika katika Jiji la Dar es Salaam.

Semina hiyo pia imehudhuriwa na mabalozi Kim Sun Pyo wa Korea na Binaya Srikanta Pradhan wa India ambapo mawakala hao pamoja na mambo mengine, wamepewa mafunzo kuhusu teknolojia mpya ya LG na baadaye wakashiriki katika kipindi cha maswali na majibu huku zawadi kemkem zikitolewa kwa waliojibu vizuri maswali hayo.
Watendaji na wafanyakazi wa kampuni hiyo pia walihudnuria kweye semina hiyo.