×

DC Kilombero Azindua Msimu Mpya Wa Uzalishaji Kiwanda Cha Sukari Kilombero

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero baada ya kushiriki kwenye uzinduzi wa msimu wa uzalishaji katika kiwanda cha K1.

 

JUNI 19, 2023, Kampuni ya Sukari Kilombero ilizindua msimu wa uzalishaji kwa mwaka 2023/24 katika moja ya viwanda vyake (K1) kwenye hafla iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya akiwasalimia wafanyakazi wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero kabla ya kushiriki kwenye uzinduzi wa msimu wa uzalishaji katika kiwanda cha K1.

 

Hafla hiyo fupi, imefuata baada ya ufunguzi wa msimu wa kiwanda cha K2 uliofanyika tarehe 14 Juni 2023 ukiashiria kuanza kwa kipindi muhimu cha uzalishaji wa sukari, ambapo kampuni inatarajia kuzalisha tani 129,080 za sukari kwa msimu.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya akiwasalimia wafanyakazi wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero kabla ya kushiriki kwenye uzinduzi wa msimu wa uzalishaji katika kiwanda cha K1.

 

Kufuatia uzinduzi wa msimu wa uzalishaji, kampuni pia itachangia katika kuzalisha fursa za ajira za msimu, kwa kuajiri wafanyakazi wa ziada kutokana na ongezeko la kazi katika msimu wa uzalishaji.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya akiweka miwa kwenye mtambo kuashiria uzinduzi wa msimu wa uzalishaji kwa mwaka 2023/24 katika kiwanda cha K1.

Leave a Comment