×

Mdau Ashirikiana na Bodaboda Kujenga Choo, Afichua Mipango Yake – Video

Katika kile kinachoonekana ni kuwasaidia vijana wenzake wa Muheza, Hamisi Sadiki Rajabu amekamilisha ndoto ya siku nyingi ya Waendesha Pikipiki maarufu Bodaboda wa Muheza.

Akiwa katika Kata ya Mlingano Wilayani Muheza leo Jumamosi tarehe 24 Juni, 2023, Hamisi ametimiza ahadi yake ya kukamilisha mradi wa choo ambao umejengwa kwa nguvu za Bodaboda hao.

“Kama mnakumbuka niliahidi kukamilisha mradi huu kwa kuwaletea vifaa vya ujenzi pamoja na kuweka milango ya jengo hili ambalo litakuwa na manufaa makubwa kwenu kama Bodaboda wa Mlingano.”

Hamisi ameendelea kusema kuwa, wakati wote amekuwa akiwaza maendeleo ya Muheza na nia yake ni kuona vijana wa Muheza wakijikomboa kiuchumi na kuishi maisha ya ndoto zao.

Bodaboda hao ambao wameunda umoja wao na kuusajili Wilayani humo, wamemuelezea Hamisi Sadiki kama kijana wa mfano na mwenye maono na mtazamo chanya juu ya Muheza.

“Hamisi ni jembe letu na sisi vijana wa Bodaboda tunamuelewa sana, amekuwa akitupambania vijana na Muheza hii unayoiona itabadilika sana endapo watajitokeza watu wengi aina ya Hamisi “, amesema mmoja wa Bodaboda hao.

Sambamba na hilo, Hamisi amechangia matofali 150 kwenye ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Kwezitu huko Muheza.

Leave a Comment