×

Rais Samia Ateua Makamu NEC, Mkaguzi Mkuu wa Serikali – Video

Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Benjamin Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.

Pia ameteua viongozi wengine wanne wakiwemo wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Profesa Idrissa Mshoro.

Profesa Mshoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi cha pili baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza.

Taarifa iliyotolewa  tarehe 29 Juni 2023 na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Samia amesema uteuzi wa wajumbe wa NEC unaanza tarehe 1 Julai mwaka huu.

Aidha, Rais Samia amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Tifa ya Uchaguzi ambaye ameteuliwa kwa kipindi cha pili.

Amemteua Balozi Omary Ramadhan Mapuri kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ambaye naye ameteuliwa kwa kipindi cha pili.

Pia Rais Samia amemteua Dk Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Leave a Comment