Klabu ya Yanga imezindua jezi zake rasmi kwa ajili ya msimu ujao wa 2023-24 ambapo uzinduzi huo umefanyika Nchini Malawi na kukabidhiwa kwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu jezi ya klabu ya Tanzania kuzinduliwa kwenye ikulu ya nje ya nchi mbele ya Marais wawili.