×

Kambi ya Simba Uturuki Balaa Ahmedy Ally Afunguka Mazito!

SIMBA wanatarajia kwenda Uturuki kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya ndani ikiwemo Azam Sports Federation (FA) 2023/24.

Uongozi wa Simba unataka timu ipate utulivu zaidi wakati wa maandalizi na ndiyo maana wamechagua nchi ya Uturuki ambayo wanaamini itakuwa na utulivu wanaouhitaji.

Licha ya kutoweka wazi eneo watakalofikia lakini Championi linafahamu watajichimbia sehemu ambayo wanaona itakuwa rafiki kwa mazoezi mfululizo chini ya Kocha Oliviera Robertinho.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally.

Huko itafanya mazoezi kwa uhuru bila kelele ikiwa na nyota wao wa zamani na wapya na hadi sasa wanaripotiwa kumalizana na kiungo mshambuliaji Onana kutoka Cameroon na beki rasta, Fandoh Che Malone.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ametoa sababu nne ambazo zimefanya wao wachague kwenda Uturuki licha ya kuwa kuna nchi nyingine ambazo wangeweza kupata utulivu.

Ahmedy Ally alisema: “Kuhusu kambi ya Simba Uturuki. Maswali ni mengi kwa nini mnaenda Uturuki si mngebaki tuu kama wenzenu.

“Jibu ni kwamba hela ya kwenda Uturuki ipo tuu sio mpaka tuuze jezi. Pili timu ya inayoshiriki Super League lazima iwe tofauti na wengine.

“Tatu timu ya 9 kwa ubora Afrika lazima ifanye maandalizi sehemu kubwa kubwa. Nne wachezaji wetu wana hadhi ya Uturuki na Ulaya. Halafu watu wa Uturuki wamefurahi kusikia tunaenda wamesema tumelipa heshima taifa lao.”

Simba wanatarajia kuondoka mwanzoni mwa wiki ijayo kwenda Uturuki kwa ajili ya pre-season hiyo.

Stori na Issa Liponda

RAIS SAMIA AZINDUA JEZI MPYA za YANGA AKIWA MALAWI, AKABIDHIWA YAKE MOJA na RAIS wa MALAWI MOJA..

Leave a Comment