
Kampuni ya Sukari Kilombero kupitia bidhaa yake ya Bwana Sukari inatumia fursa ya maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kuonyesha bidhaa zake na kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu fursa zilizopo kutokana na uwekezaji unaofanywa na kampuni katika mradi wake wa Upanuzi.

Kwa mara ya kwanza katika maonesho hayo, wateja wanaweza kujionea sukari zilizo katika paketi ndogo za gramu 50, maarufu kama ‘Kitamtam’ ambazo zinapatikana kwa bei ya reja reja ya shilingi 200/-.
Mbali na ‘Kitamtam’, kampuni inatoa punguzo la bei katika bidhaa zote kwa wateja wanakaofika katika banda hilo. Pia kuna michezo mbalimbali ambapo wateja wanaweza kujishindia zawadi kutoka kwa Bwana Sukari.