×

Wabunge Na Viongozi Wengine Wote Waaswa Kumuunga Mkono Rais Dkt Samia

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani) leo.

Dar es Salaam, Julai 6, 2023: Wabunge na viongozi waaswa kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa bora zaidi.

Akizungumza mapema leo, jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema kuwa wabunge pamoja na viongozi wamuunge mkono na kupeperusha sera nzuri wasikae kimya na wasiwe nyuma kuhakikisha uchumi wetu unakuwa na kufanya Tanzania iwe imara.

Amesema wafanye kazi zao kwa manufaa ya nchi  kwakuwa inaongozwa na chama cha mapinduzi hivyo wapeperushe sera nzuri ili wanaotaka kurudisha nyuma washindwe kwa manufaa ya Watanzania wote na vizazi vijavyo.

Wanahabari kazini leo.

“Watu wote ambao wenye nia mbaya na nchi hii lazima tupambane nao bila kuwaogopa na kumuonea haya mtu yoyote, nchi ni yetu na kila Mtanzania ana haki ya kupambana kuhakikisha amani na utulivu tuliokuwa nao tunaendelea kuwa nao.

“Mtu aweze kuishi mkoa wowote akitaka kwenda Mwanza kwenda kufanya shughuli zake aende na akitaka kwenda mahali popote aende.

Rais anafanya kazi kubwa sana mambo mengi yalikuwa hayaendi lakini sasa hivi mambo yanaenda vizuri, wawekezaji wakubwa na wadogo wanakuja kuwekeza katika nchi yetu wakati haya yote ni matunda yaliyotokana na yeye kutembelea nchi mbalimbali kuunganisha biashara ili kukuza uchumi wa nchi yetu,” amesema Msama.

Leave a Comment