
Chuo Cha Veta Pwani ni chuo kinachotoa kozi mbalimbali ikiwemo ushonaji kuanzia levo 1 mpaka 3, umeme wa magari na majumbani, maabara pamoja na sekretari.
Pamoja na hayo imekuja na mradi mpya kutengenezea mashine ya kudalizi na kutengeneza nembo au maumbo mbalimbali kwa kutumia komputa ambayo yatawekwa kwenye mashine yoyote.

Akizungumza wakati wa maonyesho ya 47 ya biashara (sabasaba) Julai 4 Mwalimu wa chuo hicho Nestory Kayombo amesema wao hufundisha mwanafunzi kutengeneza nembo au maua mbalimbali ya pembeni na kuweka kwenye mashine ambayo inafanya kulingana na ulivyoielekeza.
“Hapa inavyoonekana hapa hii nembo ambayo tayari imeshatengenezwa unaweza ukaweka kebo au flashi na kuiamishia kwenye mashine ambayo huku unapanga kabisa uzi na upande huu mwingine zinapangwa kwa namba, inafanya kazi mpaka ikimaliza uzi au ikikata uzi au ikimaliza kazi.
“Machine hizi zinapatika Nchi tofauti tofauti lakini sisi hii tumechukua Korea hivyo tunaandaa nguvu kazi ambayo itasaidia kijana kwenda kuajiriwa na kujiajiri ili kuweza kusaidia jamii ambayo imetuzunguka,”amesema Kayombo.