×

Mamlaka ya Mapato (TRA) Yatangaza Kushusha Ushuru wa Vitenge

 

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, imeweka wazi kuwa kwa sasa imepunguza ushuru wa vitenge kutokana na umuhimu wa bidhaa hiyo.

Akizungumza na Global Tv Msemaji huyo amedai kuwa vitenge vina umuhimu sana na kabla ya kupunguza ushuru huo vilikua vikiingia nchini kimagendo kitu ambacho kilipelekea TRA kukosa mapato yanayohitajika.

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa bidhaa hii inatumiwa sana na wanawake wanapokuwa hospitali na shughuli zingine, hivyo ametoa wito wa wafanyabiashara kufanya biashara zao bila uwoga kwani kila kitu ni shwari kwa sasa.

Leave a Comment