
Dar es Salaam 19 Julai 2023: Waandishi wa habari nchini wameaswa kuandika habari za kijamii na uchunguzi ili kuipa dhamani taaluma ya habari kuliko kukimbilia habari za matukio yasiyo na msaada kwa jamii.
Hayo yamesemwa wakati wa mafunzo hayo ambayo wamepatiwa waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa habari Dar-es-Salaam DCPC, na mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Jamii forums, Francis Nyonzo ambaye amesema wameona ni vyema kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uelewa waandishi wa habari ili waweze kuandika habari zenye tija kwa jamii.

Amesema kuna mambo mengi sana yanatakiwa kuibuliwa kwenye jamii kwa kuwa wao ndio wanaosimama badala ya wananchi na kufikisha ujumbe sehemu husika,akichukulia mfano yule mtu aliyechukua video ya yule muuguzi aliyekuwa akiosha vyombo na kuanika juani na suluhisho likapatikana.
Pia amesema kupitia mafunzo hayo ya siku moja wanafanya uchachamuzi katika haki za kidigitali kwa hiyo mara kwa mara na kipindi hiki wameona waandishi wa habari ni muhimu kupata elimu hiyo.
“Leo tumefenya hayo masuala ya usalama kidigitali na tumegusia kidogo kuhusu haki za kidigitali hii ni kama sehemu ya vitu ambavyo vimekuwa tukisimamia miaka yote tumekuwa na makundi mbalimbali tukiyapatia uelewa wa masuala ya kidigitali hii kwa sababu digitali haiepukiki.

“Sasa hivi watu wengi wanaingia katika masuala ya kidigitali kama tunavyoona Sasa hivi Kuna data za mwezi wa sita,zinaonyesha kwamba vifaa milioni 34 vimeunganishwa kwa hiyo ni zaidi ya nusu ya Watanzania wameunganishwa na mtandao hivyo kuna haja ya Watanzania kufahamu namna ya kuwa salama mtandaoni.
“Kwa hiyo katika makundi ambayo tunawapa ufahamu ni waandishi wa habari tunafahamu kuwa waandishi wanawasiliana na watu wengi kwa hiyo tunatamani kuona kuna wana habari nyingi zinazohusu masuala ya kidigitali na usalama wa kidigitali kwa sababu muda mrefu watu wamekuwa wakipata matatizo kwa sababu ya kutokufahamu haki za kidigitali kutokufahamu namna ya kujiweka salama mtandaoni.
“Masuala ya utapeli yamekuwa yakiendelea kwa sababu watu hawajui namna ya kujilinda mtandaoni na tumeona madhara ya watu kununua simu zilizotumika na mtu mwingine au kuokota laini ya mtu mwingine na kuitumia bila kujua alikuwa akiitumia kwa matumizi gani, hivyo hupelekea watu kupata changamoto ya kukamatwa na polisi na Kisha kupelekwa mahakamani,” amesema Nyonzo.
Nae Katibu kutoka Chama Cha waandishi wa Habari Dar-es-Salaam, Fatma Jalala ameishukuru Jamii forums kwa kutoa mafunzo hayo na ameuomba uongozi uendelee kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari na kuyafanyia kazi na kuwa wajumbe wazuri kwa wengine.