×

Yanga Yatoa Ufafanuzi juu ya Jeraha Alilopata Mahlatse Makudubela ‘Skudu’

Winga wake Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ (kulia) akifanya yake.

Klabu ya Yanga imetoa ufafanuzi juu ya kiwango cha jeraha alilopata winga wake Mahlatse Makudubela ‘Skudu‘ aliyeumia mnamo dakika ya 7 ya mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC na kushindwa kuendelea na mchezo.

Ripoti ya awali ya daktari wa klabu hiyo, Moses Etutu inaeleza kuwa Skudu kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupewa dawa ya kupunguza maumivu.

Dkt Moses anasema kuwa baada ya saa 24 ndio wataweza kujua kama jeraha la goti alilopata ni kubwa na linahitaji vipimo zaidi au ni mshtuko wa kawaida ambao anaweza kurejea uwanjani baada ya mapumzikl ya siku 2.

“Tumempa dawa ya kukata maumivu na anasema anajisikia vizuri sasa, lakini ni ngumu kusema kuwa yuko sawa mpaka saa 24 zitakapopita, hapo ndio tutajua kama goti lake limedhurika kwa kiasi gani,” alisema Dokta Moses

Na Ibrahim Mussa

MUNGU WANGU! FIGO ZIMEFELI, ANA UVIMBE TUMBONI, AMEZUNGUKA KOTE HAPONI, AWALILIA WATANZANIA

Leave a Comment