×

Rais Samia Awataka Mabalozi Kufuatilia Hati Za Makubaliano Zilizosainiwa -(Picha + Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Rais Samia akimuapisha Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, kuwa Balozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Rais Samia akimuapisha Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Bw. Hassani Iddi Mwamweta kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

 

Mabalozi Wateule wakila Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

Amesema “Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu. Nilikutana na Rais mwenzangu ndani ya #SADC akaniambia nimbadilishie Balozi kwa kuwa aliyepo kazini haendi na mikutano hashiriki.”

Amesisitiza baadhi ya Mabalozi hawatoi ripoti muhimu katika maeneo yao, ndio maana aliunda Kamati ya kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ili kubaini mambo kadhaa ikiwemo kasoro, mazuri na ugawaji wa Mabalozi

Amesema “Mnapokwenda angalieni tumesaini nao kitu gani na vimefikia hatua zipi, mnapopeleka Hati za Utambulisho mkikaa na Rais au Mfalme wa Nchi husika zungumzeni mawili matatu ambayo yametekelezwa au yapo njiani.”

CHOTA MAPENE ndiyo mchongo mpya town! Kwa shilingi 1,000 tu, yaani BUKU unajichotea mapene kibao au kupata nafasi ya kujishindia ZAWADI MBALIMBALI KILA SIKU, KILA WIKI kupitia Global TV, Global Radio na mitandao ya kijamii! ======================== Ingia kwenye simu yako📲, sehemu ya kufanyia malipo, andika namba ya kampuni 553111, kumbukumbu namba 255 au andika neno GLOBAL. Weka kiasi cha shilingi 1,000, weka namba yako ya siri, thibitisha na tuma.👍 PEASA UTATUMIWA MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO!🤝👍💰

Leave a Comment