×

Msanii Chino Alivyonogesha Promosheni ya Jipatie Infinix

“Natumia Infinix Note 30 picha zangu na video zangu mitandaoni zimekuwa na ushua mwingi tangu nimekuwa mwanafamilia wa Infinix” ameyazungumza hayo Msanii wa Kizazi kipya Chino Kiddy hapo jana wakati wa uzinduzi wa promosheni ya JIPATE NA INFINIX pia amewataka mashabiki zake na watanzania kwa ujumla kununua simu za Infinix kwenye maduka yaliyopo karibu yao kwani huu ni mwezi wa kujipatia mazawadi mengi mno.

Haikuishia hapo Chino aliongea kuhusu music wa Amapiano “sio poa kuonyesha chuki kwenye music wa Amapiano ni sawa na kuweka chuki kwenye ridhiki ya mtu wapo Madj wakali wanafanya vizuri kupitia amapiano”.

Chino aliwaaga mashabiki na wateja kwa burudani ya music akiwa na wanae lakini pia balozi wa promosheni hii Frida Amani baada ya kuulizwa nini kinatofautisha simu za makampuni mengine na simu za kampuni ya Infinix alidai kuwa “simu za Infinix hazina makwanzo kwenye swala zima la chaji natumia Infinix nimeepukana na kero za simu kuisha chaji kiholelaholela tangu nimeanza kutumia Infinix NOTE 30 nipo mtandaoni muda wote.”

JIPATE NA INFINIX ni promosheni ya mwezi mzima na inafanyika kwa mikoani kote ndani ya msimu huu wa JIPATE NA INFINIX ukinunua Infinxi NOTE 30 Series, HOT 30 series, Zero Ultra au Smart 7 utajiweka katika nafasi ya kuzawadiwa Jokofu, pikipiki, laptop au Microwave lakini pia zawadi nyingine nyingi hutolewa papo hapo vilevile unaweza nunua Infinix note 30 kwa mkopo bila ya kutozwa riba.

Tembelea @infinixmobiletz au piga namba 0659987284 kwa huduma ya haraka.

Leave a Comment