×

Makalla aitaka Pamba ligi kuu, Aomba umoja kwa wana Mwanza

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameomba wadau na wanamichezo kote mkoani Mwanza kujitokeza kuipa nguvu timu hiyo ili malengo ya kucheza Ligi kuu msimu ujao yaweze kutimia.

Mkuu huyo wa mkoa  ametoa kauli hiyo leo baada ya kuitembelea timu ya Pamba jiji mazoezini  na kuzungumza na wachezaji na uongozi wa timu hiyo,Makalla amesema Pamba Jiji FC sasa ipo katika mikono salama na mipango inaendelea ya kuhakikisha timu hiyo inacheza ligi kuu kwa msimu ujao wa ligi.

Makalla ambaye pia ni mlezi wa wana TP LINDANDA WANAKAWEKAMO kama inavyojulikana na mashabiki wake,amebainisha kuwa malengo ya Pamba jiji fc  kupanda Ligi kuu yanakwenda na mshikamano wa pamoja

“Nitoe wito kwa wana Mwanza wote hii ni timu yao ambayo sasa ipo chini ya Halmashauri yetu ya Jiji la Mwanza, naomba kuchukua nafasi hii kuwaomba watu binafsi na mataasisi  mbalimbali waje kuwekeza katika timu hii kwakua malengo yake ni kupanda daraja na ili tupande lazima kila mmoja ashiriki kuona Mwanza tunakuwa na timu ya ligi kuu ,” alisema  Makalla.

Makalla ambaye amewahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu  miaka ya nyuma amewataka wachezaji kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuonesha bidii dimbani na kutanguliza nidhamu ili Pamba jiji iweze kufanikiwa. Wote tuna Imani kuwa Pamba Jiji FC ipo katika mikono salama hasa baada ya kuimarisha benchi la ufundi chini ya kocha wake mkuu  Mbwana Makatta anayesaidiwa na Renatus Shija ” alisema

Mbali na mkuu huyo wa mkoa kuitembelea timu hiyo kuona maziez kwa mara ya kwanza tangu ibadilishwe umiliki wake aliwapatia motisha ya Shilingi za kitanzania milioni moja (1000,000) iliyoungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mwanza (MZFA) Vedastus Lufano aliyetoa kiasi kama hicho.

Mhe.Mkuu wa Mkoa tumepokea maagizo yako yote na tutahakikisha tunafikia malengo ya kucheza Ligi kuu msimu ujao,tunafarijika tuna timu nzuri na inaendelea kuimarishwa,”Sima Costantine Sima,Meya wa Jiji

Kwa upande wake Kocha mkuu wa Pamba jiji Mbwana Makata amempongeza mkuu huyo wa mkoa kwa kutembelea mazoezi ya timu hiyo ambapo amesema kuwa “timu yetu kwa sasa inamchanganyiko wa wachezaji wazawa na baadhi waliotoka nje ya Mwanza,tunaendelea kufanya mazoezi na mchujo ili tuje kupata

Leave a Comment