
Meneja mkongwe katika soka la Italia Carlo Mazzone (86), amefariki dunia.
Mazonne aliwahi kuzichezea Roma, Latina, SPAL, Siena na Ascoli katika miaka ya 1950 na 1960.
Baadaye aliingia kwenye uongozi na kusimamia klabu nyingi zikiwemo Ascoli, Fiorentina, Roma , Bologna na Napoli.
Mwaka 2006, baada ya miaka 38 ya usimamizi wa soka alistaafu.
Wadau mbalimbali wa soka akiwemo Gianluigi Buffon wametuma salamu zao za rambirambi kufuatia kifo cha mwanasoka huyo.