×

Dk. Alex Malasusa Achaguliwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)

Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amechaguliwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) akichukua nafasi ya Askofu Dk. Frederick Shoo.

Malasusa amewashinda Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara na Askofu Dkt. George Fihavango.

Askofu Dkt Malasusa anarejea kwenye KITI hicho kwa mara nyingine, aliwahi kuwa Mkuu wa KKKT kwa vipindi viwili, kabla ya kumpisha Askofu Dk. Shoo.

Leave a Comment