
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) imetangaza, Emmerson Mnangagwa kuwa ametetea Kiti chake kwa 53% ya Kura zilizopigwa.
ZEC imesema Mpinzani Mkuu wa Mnangagwa, Nelson Chamisa anayeongoza chama cha Citizens’s Coalition for Change (CCC), alipata 44% ya kura za Urais, hata hivyo Chamisa amekataa Matokeo hayo.
Hatua hii inakuja ikiwa ni muda mfupi tangu Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU OEM) kutangaza kuwa Uchaguzi huo haukuwa Huru na Haki, huku baadhi ya Waangalizi wa Uchaguzi huo wakikamatwa
Mnangagwa aliingia Madarakana mara ya kwanza mwaka 2017 kwa kumpindua Robert Mugabe.