×

Tanzania Yatajwa Kuwa Chanzo Cha Baraka Kufuatia Amani, Utulivu, Rasilimali Na Uongozi Bora

Dar es Salaam, 5 Agosti 2023: Taifa la Tanzania limetajwa kuwa chanzo cha baraka kufuatia amani, utulivu na rasilimali za nchi kutokana na uwepo wa uongozi unaozingatia haki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi alisema  inatakiwa Watanzania kujua jinsi nchi ya Tanzania ilivyobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa rasilimali za kutosha.

Halisi alisema inatakiwa Watanzania wajitambue na  kubadilisha mienendo yao  kwa kuhakikisha wanakuwa baraka kwa wengine.

“Kwa kuwa Tanzania imebarikiwa, Watanzania  wanapaswa kubadilisha mienendo yao kwa kuchangua namna bora ya kuishi ili kuendelea kuwa baraka kwa mataifa mengine,” alisema

Halisi alisema kanisa hilo limekuwa likiishi kwa kuhimiza amani, upendo, kuzalisha haki  ndio maana limeandaa mkutano wa kijamii  utakaofanyika Septemba 10, jijini Dar es Salaam na zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya nchi  watashiriki.

Alisema mkutano huo utabebwa na mada isemayo Tanzania ndiyo chanzo cha baraka kwa mataifa yote lengo ni kuwapa uelewa Watanzania kuzitambua rasilimali zilizopo.

“Kanisa hili ili kuhakikisha rasilimali zinalindwa  ikiwepo amani, upendo  na kuzalisha haki, tumekuwa  na desturi ya kila siku saa 11 asubuhi kuwaombea viongozi waliopo madarakani  wazidi kuongoza kwa haki,”alisema.

Leave a Comment