×

Huu Ndio Upekee Wa TECNO CAMON 20 Ya Doodle

TECNO imeachia matoleo mawili ya CAMON 20 Series kwa Mwaka huu ambapo sanaa ya Bw Doodle imetumika katika kuleta utofauti kati ya toleo hili jipya na CAMON 20 series ya awali. CAMON 20 yaBw. Dooble hubadilika badilika rangi na kung’aa nyakati za usiku na kuonyesha michoro ya Bw. Doodle kama inavyoonekana pichani kitu ambacho huezipata kwenye toleo la awali la CAMON 20.                                TECNO imeshirikiana na mtu wa Sanaa Bwana Sam Cox almaarufu Mr Doodle katika kuleta Sanaa hii kwenye simu za CAMON 20.

CAMON 20 ya Doodle hufyonza mwanga wakati wa mchana na kuiachilia kama umeme wakati wa usiku, na hivyo kuruhusu sehemu ya nyuma ya simu kuonyesha kazi za graffiti za Mr Dooble. Muundo wa kipekee wa toleo la mfululizo wa CAMON 20 la Bw Dooble huifanya kuwa aikoni ya mitindo wakati wa mchana na kuvutia macho wakati wausiku na kuifanya kuwa bora kabisa inayochanganya mitindo na Sanaa na hii ndio tofauti kubwa kati ya TECNO CAMON 20 Mr Doodle na simu nyingine.

TECNO CAMON 20 premier doodle edition wakati wa usiku.                                                                                      

Vilevile TECNO CAMON 20 Toleo la Dooble ina mandhari iliyogeuzwa kukufaa kwa mtindo wa grafiti ya Bw. Dooble, AR SHOT na AOD, kuleta mshangao zaidi kwa mtumiaji wakati wa uchukuaji picha.

TECNO CAMON 20 pro na TECNO CAMON 20 Premier zinaashiria maana halisi ya ubunifu na mabadiliko ya teknolojia kimuundo na kiutenda kazi, umahiri wa uchukuaji picha katika nyakati mbalimbali ni wenye ubora unaonekana kupitia picha na video za camera ya simu hizi.

TECNO CAMON 20 Pro 5G Dooble ina camera kuu ya Mega pixel 64 nyuma (Night Potrait Master), 32MP Selfie Camera, 33W flash charge 5000mAh, 256GB ROM + 8GB RAM.

CAMON 20 Premiere 5G Doodle ina camera kuuya Megapixel 108 wide angle (Night Portrait Master), 32MP Selfie Camera, 45W flash charge 5000mAh, 512GB ROM + 8GB RAM.

Leave a Comment