×

Kampuni Ya Oryx Energies Yawekeza Katika Ugavi Na Usambazaji Wa LPG Zanzibar

Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Limited, Benoit Araman akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Unguja Zanzibar wakati kutangaza kuungana kwa makumpuni ya gesi ya Oryx Gas Zanzibar Limited na TP Company Limited ya Zanzibar ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies ili kuwezesha wakaazi wa Zanzibar kupata nishati safi ya LPG kwa gharama nafuu.

Mji Mkongwe Zanzibar, Tanzania na Geneva, Uswisi, Septemba 15, 2023: Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited imeungana na kampuni ya TP Company Limited ya Zanzibar, ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies (Vigor Group), ili kuimarisha ugavi na usambazaji wa gesi ya LPG (liquefied petroleum gas) katika visiwa hivyo.

Hatua hiyo inafuatia uundwaji wa kituo cha kwanza cha gesi ya LPG visiwani, Ikiwa ni sehemu ya dhamira pana ya Oryx Energies Group kutimiza ajenda ya mpito ya nishati, ambayo inahusisha kuhakikisha upatikanaji wa gesi hiyo kwa masoko ya Afrika na hasa kwa Tanzania bara na visiwa vya Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vigor Group, Abdallah Salim Turky akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Unguja Zanzibar wakati kutangaza kuungana kwa makumpuni ya gesi ya Oryx Gas Zanzibar Limited na TP Company Limited ya Zanzibar ambayo ni kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies ili kuwezesha wakaazi wa Zanzibar kupata nishati safi ya LPG kwa gharama nafuu.

Katika makubaliano yenye sehemu mbili, TP Company Limited ikisaidiwa na Oryx Energies inajenga kituo cha kwanza kabisa cha LPG Zanzibar, chenye uwezo wa MT 1,300. Kituo hicho kinatarajiwa  kukamilika katika robo ya nne ya mwaka 2023, kituo hiki kipya kitaendeshwa na kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited pekee kwa muda mrefu, na hivyo kuhakikisha ubia wa kudumu.

Wakati huo huo, Oryx Gas Zanzibar Limited itakuwa inanunua 100% ya mali za biashara ya LPG za TP Company Limited, ambazo kwa sasa zinatambulishwa na kuendeshwa kwa jina la VGas. Mali hizi zitabadilishwa na kuwa chini ya jina la Oryx Energies hatua kwa hatua. Kwa upande wake, TP Company Limited inachukua asilimia 30 ya hisa za Oryx Gas Zanzibar Limited. Makubaliano haya yatakuwa na sifa za kipekee, yakiweka mwanga kwa dhamira ya Oryx Energies kama kampuni kusaida mipango ya jamii na kukuza ushirikiano wa ndani.

Mmoja wa wadau akizungumza kwenye mkutano huo.

Ikiwa kampuni ya uendeshaji wa kituo kipya cha LPG, Oryx Gas Zanzibar Limited itawasambazia gesi wateja wengine pia, na hivyo kusaidia kuhakikisha upatikanaji wa gesi ya uhakika, endelevu na usio na vikwazo kwa wakazi wa Zanzibar. Hatua hiyo pia inashughulikia hali ngumu ya kihistoria ya usambazaji wa ndani wa gesi ya kupikia, ambapo taratibu nyingi za uendeshaji na usimamizi zimeongeza gharama kwa Wazanzibari na mara nyingi kusababisha vikwazo.

Shuwekha Khamis, Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Limited, alisema: “Maendeleo haya ya ushirikiano na kampuni kubwa ya ndani ya nchi yanahakikisha dhamira yetu kuwapatia wakazi wa eneo hili nishati safi ya kupikia. LPG ina nafasi kubwa katika mchanganyiko wa nishati Zanzibar, na inahakikisha usalama wa nishati muhimu ya kupikia na pia kusaidia maendeleo ya sekta ya utalii wa ndani.”

Benoit Araman, Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Limited, aliongeza: “Kwa muda mrefu tumekuwa tukijenga misingi ya upanuzi huu, baada ya kufikisha LPG katika visiwa vya Zanzibar tangu mwaka 2010, ushirikiano huu ni hatua muhimu ya kuimarisha zaidi usambazaji wa gesi ya LPG Zanzibar.”

Abdallah Salim Turky, Mkurugenzi Mtendaji wa Vigor Group, alisema: “Kuundwa kwa kituo kipya cha LPG kunaendana kikamilifu na maono yetu ya kuwa mstari wa mbele katika kutoa bidhaa na huduma za hali ya juu ndani ya nchi kutoka kwa masoko ya kimataifa kufikia jamii yetu kwa bei wanazoweza kumudu.

Hii itasaidia kuboresha viwango vya afya na ustawi wa Zanzibar na pia itasaidia kulinda mazingira kwa kutoa njia mbadala, salama na ya uhakika kwa matumizi ya mkaa na kuni.” Aliongeza: “Ili kufanikisha hili, tunayofuraha kuingia ubia na Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited, Kampuni na timu nzima imejijengea sifa na umaarufu kama mshiriki anayetambulika vyema kwenye soko la rejareja.

Kutoka kushoto kwenda kulia: Toufiq Salim Turky (Mwenyekiti wa Vigor Group), Benoit Araman (Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Limited), Shuwekha Omar Khamis (Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Limited), Abdalla Salim Turky (CEO wa Vigor Group).

Kuhusu Oryx Energies

Oryx Energies ni moja ya makampuni makubwa na ya muda mrefu zaidi ya utoaji wa bidhaa na huduma za nishati barani Afrika.

Oryx Energies huhifadhi na husambaza bidhaa za nishati zinazohitajika na watumiaji, biashara na shughuli za baharini, ikiwa ni pamoja na mafuta, gesi ya LPG na vilainishi, na pia inatoa huduma za maeneo maalum ya hifadhi. Ikijikita kwenye kushughulikia mahitaji yanayobadilika ya bara la Afrika kwa miaka 35, Oryx Energies inanufaika kutokana na uzoefu wa kina, maarifa na utaalam, uliokusanywa katika kuhudumia mahitaji ya nishati ya nchi zaidi ya 20.

Kuhusu Oryx Gas Zanzibar

Oryx Gas Tanzania imekuwa ikifanya kazi katika usambazaji wa LPG tangu mwaka 2001. Ilianza kusambaza mitungi ya LPG kwa Zanzibar mwaka 2010 na imeendesha bohari kuu ya kuhifadhia tangu 2017.

Mnamo 2021, Oryx Gas Zanzibar iliandikishwa. Tangu wakati huo imejikita kutoa suluhisho la nishati ya LPG katika visiwa vya Zanzibar. Oryx Gas Zanzibar inaendelea kutangaza nishati safi ya kupikia na kujenga ufanisi na uhakika wa upatikanaji wa nishati katika sekta muhimu kama vile utalii.

LPG ni chanzo mbadala cha nishati ya kupikia kinachotumika kwa mahitaji ya majumbani, kibiashara na viwandani.

Wasiliana nasi

Kwa mawasiliano Oryx Energies

Barua pepe: [email protected]

Tovuti: https://www.oryxenergies.com#

Tufuate kwenye LinkedIn / Facebook: @OryxEnergiesHQ @OryxEnergiesTanzania

Kuhusu TP Company

Kampuni ya TP ilianzishwa mwaka 2012. Ilianza usambazaji wa LPG mwaka 2017 katika Visiwa vya Zanzibar na ina kiwanda cha kujazia gesi kilichopo Mangapwani chenye eneo la kuhifadhia gesi hiyo. Mradi unajivunia kujikita moja kwa moja katika biashara ya usambazaji wa LPG.

Dira ni kuisaidia Zanzibar na wakaazi wake kupata nishati safi zaidi kwa bei nafuu.

Wasiliana nasi

Nambari ya simu: +255 242230722

Barua pepe: [email protected]

Tovuti: https://www.turkysgroup.co.tz

Leave a Comment