×

Wanafunzi Saba wa Sekondari Mbaroni Kwa Kuwafanyia Wanafunzi wa Msingi Mtihani wa la 7

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewahoji watu saba kwa tuhuma za kosa la udanganyitu wa mitihani ya darasa la saba kwa kuwachukua wanafunzi wa sekondari na kuwafanyisha mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wa darasa la saba.

Tukio hilo lilitokea tarehe 13.09.2023 muda wa saa nane mchana huko katika shule ya msingi lgulumuki, kata ya lgulumuki, tarafa ya Sengerema wakati kamati ya mitihani ya wilaya ya Sengerema ilipotembelea shule hiyo kwa ajili ukaguzi na kubaini kufanyika kwa udanganyifu huo ambapo mkondo namba mbili na namba tatu kulikuwa kumeingizwa wanafunzi wa sekondari watatu na kufanya mitihani ya darasa la saba.

Watuhumiwa waliokamatwa na wanaendelea kuhojiwa ni
1.Maiko Sheusi, miaka 35, mwalimu wa shule ya Sekondari Sima ambaye ni msimamizi mkuu wa mihani shule ya msingi Igulumuki
2.Musa mwashihava, miaka 38, mwalimu wa shule ya sekondari Kilabela ambaye ni msimamizi wa mtihani mkondo namba 2,
3 Bonasi Balozi, miaka 33, mwalimu wa shule ya sekondari Buzilasoga ambaye alikuwa msimamizi wa mihani mkondo namba 3,
4 Azizi Mohamed, miaka 36 ,Mwalimu wa taaluma, shule ya msingi Igulumuki ,
5 Shadrack Bwana, miaka 14, mwanafunzi wa shule ya sekondari Sima,
6 Revocatus Paulo, miaka 14, mwanafunzi wa shule ya sekondari Sima.
7. Pendo Bukoma, miaka 14, mwanafunzi wa shule ya sekondari Sima, mkazi wa lqulumuki.

Kufuatia tukio hilo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igulumuki aitwaye Amlesian Mahingu Mfungo aliweza kukimbia mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na jitihada za kumsaka ili aweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya upelelezi kukamilika. Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza pamoja na kutoa elimu, pia limeendelea kuimarisha ulinzi maeneo yote na halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wahalifu.

MASKINI MTOTO BAKARI (5) ANAPITIA MATESO MAKUBWA – MAMA YAKE ALIA – “IMELAZIMU ATOBOLEWE TUMBO”…

Leave a Comment