×

Nafasi za Kazi Global Publishers; Maofisa Mauzo Wenye Uzoefu Wa Kutafuta Masoko

GLOBAL PUBLISHERS AND GENERAL ENTERPRISES LIMITED, ni kampuni ya uchapishaji magazeti na wamiliki wa Global TV, Global Radio na mitandao yake ya kijamii inayofuatiliwa na watu wengi ndani na nje ya nchi.

Kampuni inawatafuta MAOFISA MAUZO wenye uzoefu wa kutafuta masoko kwenye vyombo vya habari (utafutaji wa Matangazo), wenye ujuzi na sifa zifuatazo.

SIFA:
-Wawe wameshawahi kufanya kazi kwenye vyombo vya habari idara ya matangazo, au wawe wameshawahi kufanya kazi na Kampuni za Mawakala wa Utangazaji (Advertising Agency), kwa muda usiopungua miaka miwili.

-Wawe na uzoefu wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza na wawe wanaishi jijini Dar es Salaam.

Pia tunakaribisha maombi ya watu wenye uzoefu na masuala ya matangazo kuomba kama FREELANCERS, ndani na nje ya Dar es Salaam.

Leave a Comment