×

Waliosoma Lugoba Sekondari Watoa Msaada Kuboresha Hadhi ya Shule hiyo

Ili  kuhakikisha Shule ya Sekondari LUGOBA iliyopo  halmashauri ya wilaya Chalinze mkoani Pwani inarejea katika makali yake kitaaluma, nidhamu na heshima iliyojengwa siku za nyuma, baadhi ya wadau mbalimbali waliowahi kusoma shuleni hapo wametoa msaada wa vifaa mbalimbali kukarabati baadhi ya majengo.
Umoja wa wanafunzi hao unaotambulika kwa jina la LUGOBA UNITY wamekabidhi
Seti ya mashuka  20 katika halmashauri ya Wilaya ya chalinze kituo Cha Afya Cha Lugoba pamoja na  Makabati Yakuhifadhia mashine za nukta nundu kwa ajili ya  watoto wasiona.
Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa LUGOBA UNITY Thomson Sanga amesema sehemu kubwa ya malengo yao ni kukusanyana na kuisaidia shule hiyo kutokana na wataalam mbalimbali waliozalishwa shuleni hapo mpaka sasa.
Naye Msemaji wa Lugoba Unity Virginia Naina amewataka wanafunzi kudumisha nidhamu, kuzingatia masomo, kuweka ushindani chanya kwenye masomo ili kuipaisha shule yao kwani miaka ya nyuma shule hiyo ilisifika kwa ufaulu mzuri, heshima na bidii katika masomo.
Naye Mwalimu Mkuu  wa shule hiyo  Abdallah Sakasa Amewaomba wanafunzi hao waliomaliza Kuendelea Kudumisha amani na mshikamano huku Mjumbe wa BODI ya Shule God Mwaibalaamewashukuru wote wanaoendelea kuisaidia shule yao.
Kwa upande wa Mwanafunzi wa kidato Cha sita katika shule hiyo IRENE NGERANGERA alikuwa na haya ya kusema….

Leave a Comment