×

Mo Music Nimehitimu, Sasa Kazi tu

mo musiccccMoshi Katemi ‘Mo Music’

Stori: Mayasa Mariwata 

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake mpya wa Skendo, Moshi Katemi ‘Mo Music’ ameahidi makubwa baada ya kuhitimu shahada ya Mahusiano ya Umma na Masoko katika Chuo Kikuu cha St. Augustine kilichopo Mwanza.

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Mo Music alisema alikuwa akipata changamoto kubwa kutenga muda wa kufanya muziki na kusoma na kufunguka kuwa kwa sasa amemaliza jukumu moja hivyo ana muda mzuri wa kufanya muziki.

“Nimemaliza rasmi shahada yangu pale St. Augustine sasa nitakuwa na nafasi yakufanya muziki hivyo mashabiki wangu wakae mkao wa kupokea nyimbo kali zaidi,” alisema Mo Music.

Leave a Comment