
Zanzibar 29 Oktoba 2023: Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wananchi kufanya mazoezi kwa lengo la kujenga afya imara ili kupunguza maradhi yasiyoambukiza ambayo yameonekeana kuongezeka visiwani Zanzibar
Rais Dkt Mwinyi ameeleza hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mbio za Kimataifa za Riadha za Tigo Zantel Zanzibar ambazo zinafanyika kwa mwaka wa tatu visiwani hapa.
Amesema kwasasa watu wengi wanasumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza na kwa asilimia kubwa huchangiwa na watu kutofanya mazoezi na kula mlo uliokua bora, hivyo amewahimiza wananchi kushirki katika kufanya mazoezi ili kupambana na magonjwa hayo

Aidha amesema kufanyika kwa marathon hizo Zanzibar kutasaidia kuimarisha ukuaji wa sekta ya utalii kwa nyakati zote na kuwanufaisha wananchi wa Zanzibar kutokana na wimbi kubwa la wageni kutoka mataifa mbalimbali kuingia nchini
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Pesa kutoka Kampuni ya Tigo Zantel, Angelica Pesha amesema kampuni yao itaendelea kuendesha mbio hizo ili kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kuimarisha sekta ya utalii kupitia michezo kwa kuwa mbio hizo kwasasa zimekua maarufu ambazo huitangaza Zanzibar Kimataifa
Ameongezea kuwa mbali na hatua hiyo pia kampuni yao itaendelea kuzitumia fursa mbalimbali za uwekezaji kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali ya awamu ya nane visiwani Zanzibar
Miongoni wa washindi wa Marathon hizo pamoja na wadau wameipongeza kampuni ya TigoZantel kwa maandalizi mazuri ambayo yanakidhi viwango vya kimataifa na kuzifanya mbio hizo kukua kila mwaka na kuahidi kusaidia ufanikishaji wa mbio hizo.