×

Shija Grace Godfrey aachia video mpya “Mimi Nimebarikiwa” – Audio

Msanii chipukizi wa nyimbo za Injili nchini, Shija Grace Godfrey ameachia wimbo wake mpya uitwao, ‘Mimi Nimebarikiwa’ kupitia mtandao wa YouTube na platforms nyingine za muziki Duniani.

Mwanadada huyo ambaye anatikisa kwa sasa kwenye tasnia hiyo ya nyimbo za Injili amesema wimbo huo ni maalum kwa ajili ya kumtukuza Mungu kwa yale ambayo amemfanyia na ni faraja kwa wale wanahisi kukata tamaa kwani Mungu wanayemtegema yupo kazini, hatowaacha kamwe.

Sikiliza wimbo huo ubarikiwe.

Leave a Comment