Hali ya taharuki imeibuka mkoani Iringa mara baada ya mama ntilie na mteja wake wa kiume kukutwa wamefariki wakiwa watupu.
Global Tv imefika katika eneo la tukio na baadhi ya majirani kuiambia Global Tv kuwa huenda watu hao walizidiwa na moshi wa maharage kwani walikuta maharage yamebandikwa jikoni.
Majirani wameendelea kuiambia Global Tv kuwa ijapokuwa wamekutwa wamefariki lakini hawana majeraha katika miili yao na hivyo wanangoja polisi wafike kufanya uchunguzi ili watoe majibu yenye usahihi.