
Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu amteue Mwenyekiti wa Bodi hiyo
Kwa mujibu taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais amefanya uamuzi kuanzia Novemba 7, 2023
Waliokuwa Wajumbe wa Bodi hiyo ni Mhandisi Othman S. Khatib (Mwenyekiti), Khalfan S. Saleh (Makamu Mwenyeki), Mzee S. Mndewa (Mjumbe), Fatuma S. Ikuja (Mjumbe), Abdallah B. Katunzi (Mjumbe) na Rehema J. Khalid (Mjumbe)
