×

Mauaji Ya Kutisha Sudan, 700 Wauawa Darfur

Wapiganaji wa Kundi la Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, wamevamia kambi za wakimbizi na vijiji kadhaa Magharibi mwa Darfur na kufanya mauaji ya halaiki na makubwa zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Inaelezwa kwamba takribani watu 700 wameuawa, huku wengine wakieleza kwamba waliofariki dunia wamefika 1,300 na wengine 2,000 kujeruhiwa huku 310 wakiwa hawajulikani walipo.

Montesser Saddam, mmoja kati ya manusura wa mauaji hayo aliyefanikiwa kukimbilia nchini Chad, ameeleza kuwa walikuwa wakipita nyumba kwa nyumba na kuwapiga risasi wanaume na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wanawake, ikiwemo kuwabaka.

Inaelezwa kuwa machafuko yanayoendeshwa na RSF, ni sehemu ya kampeni chafu ya kuwaua na kuwamaliza wananchi wa kabila la Masalit, Darfur.

Tangu kuanza kwa machafuko nchini Sudan, April mwaka huu, Umoja wa Mataifa na Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakikemea vikali machafuko hayo yenye sura ya ubaguzi wa kikabila, Kabila la watu weusi la Masalit likilengwa zaidi.

Leave a Comment