×

Rais Samia Afanya uteuzi Bodi ya Wakurugenzi wa TCRA

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dkt. Jones Killimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCRA.

Pia Rais Samia amemteua Juma Hassan Reli kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCRA.

Leave a Comment