
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Godfrey Chongololeo Jumanne Novemba 21, 2023 amezungumza na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi Wazawa, Washauri Waelekezi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi wa kujadili nafasi yao katika utekelezaji wa miradi na masuala yanayohusu sekta hiyo, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.