×

#UPDATES: Watu 13 wafariki na wengine 36 Kujeruhiwa baada ya basi la Ally’s Star kugonga treni

Watu 13 wamefariki dunia na wengine 36 wakijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ally’s Star lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga treni ya mizigo katika makutano ya barabara na reli maeneo ya Manyoni mkoani Singida.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dkt. Furaha, amethibitisha taarifa hizo na kwamba majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika Hospitali za Itigi Mission na Hospitali ya wilaya ya Manyoni.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Novemba 29, 2023

Leave a Comment