×

Mke Atuhumiwa Kuua Mume Wake Kwa Kumchoma Kisu Iringa, Kisa Chadaiwa Wivu Wa Mapenzi – Video

Mwanamke Mmoja aliyejulikana kwa jina la Fadhila Balama wa Mtaa wa Kitwiru A Manispaa na wa Mkoani Iringa anatuhumiwa Kumchoma na kitu chenye ncha kali Mume wake Denis Chumbula hadi kupelekea kifo mara baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Mjomba wa Marehemu Denis Chumbula anayeitwa Victor Kihaga amesema alipokea taarifa za Mpwa wake kuchomwa na kitu chenye ncha kali kutoka kwa majirani na baada ya kufika alikuta Marehemu anavuja damu.

Alichukuwa hatua ya kumpeleka hospitalini kupatiwa matibabu na ilipofika November 28, 2023 umauti ulimkuta.

Leave a Comment