
Gwiji wa Tennis Duniani John McEnroe usiku wa kuamia leo Desemba 3, 2023, yeye na familia yake na wadau wengine zaidi ya 80 kutoka Marekani wameungana na wadau wa utalii nchini kwa kushiriki chakula cha usiku kilichoandaliwa na Wizara ya Utalii chini ya Mhe Waziri Angellah Kairuki jijini hapa akisisitiza kuipenda Tanzania kwani imejaaliwa raslimali nyingi na ni nchi nzuri.
Disemba 5 mwaka huu Serengeti gwiji huyo namba moja duniani mara nne katika Tennis enzi zake na mdogo wake Patrick McEnroe watatoana jasho katika mchezo mkali wa kimataifa wa hisani ikiwa ni mara ya kwanza Tennis kuchezwa kutokea hifadhi hiyo na kutazamwa kote duniani.
