
Mshindi wa Kampeni ya Serengeti Lite ‘Maokoto Ndani ya Kizibo’ Kibaha mkoani Pwani, Advocatus Kakorozya, Jumamosi Desemba 2 mwaka huu amekabidhiwa okoto lake la shilingi laki tano baada ya kuibuka mshindi wa kanda hiyo.
Advocatus alikabidhiwa okoto hilo na Mkuu wa Usimamizi wa Bia za Serengeti Kanda ya Kibaha Pwani, Omary Zavallah kwenye hafla iliyofanyika kwenye Bar ya Up Date iliyopo Kibaha Kwa Mfipa na kuhudhuria na umati mkubwa watu.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa maokoto yake aliyojishindia, Advocatus alisema siku zote amekuwa mpenzi mkubwa sana wa bia za kampuni ya Serengeti na sehemu yake kubwa ya kupumzika na kupata kinywaji ni maeneo ya Kibaha Kwa Mathias.

Mshindi huyo amesema hivi majuzi akiwa anapata kinywaji maeneo hayo kama kawaida yake tangu kuanzishwa kampeni hii anaponunua bia za Serengeti anachukua namba zilizopo chini ya kizibo na kuzituma kwenda namba *150*80# kisha ok.
Advocatus amaesema baada ya kutuma namba hizo alirudishiwa ujumbe kuwa ameingia kwenye droo ya Serengeti Maokoto Ndani ya Kizibo na baada ya hapo ndipo alipopigiwa simu ya kuambiwa kuwa yeye ndiye mshindi wa kampeni hiyo Kanda ya Kibaha. Aliendelea kusema;

“Tangu ianze kampeni hii nimekuwa nikifanya hivyo na kupata ushindi wa pesa ndogondogo lakini sikuchoka kushiriki lakini leo nashukuru kuibuka na ushindi huu wa laki tano.
“Kwa ushindi ni kama bia zote nilizokuwa nikinywa mwezi mzima nilikuwa nikinywa bure na chenji nimerudishiwa hivyo nawashauri wanywaji wengine kutumia bia za kampuni hii ambayo inatujali wateja wake kwa kuturudishia sehemu ya faida tunayowapa”. Alimaliza kusema mshindi huyo.
Naye Msimamizi wa Bia za Serengeti Kanda ya Kibaha, Omary Zavallah amewata wanywaji wa bia pote nchini kutumia bia za kampuni hiyo ambazo katika kujali afya za wateja wake hazina sukari na unapotumia huamki na uchovu kama bia zingine.
Zavallah amewataka wanywaji nchi nzima kuendelea kushiriki promosheni hiyo kwa wingi kwani zawadi bado zipo za kutosha na zinatolewa kila kona.