
Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Kupitia programu yake inayojulikana kama ‘Code Like a Girl’ kwa kushirikiana na Tanzania Data Lab (dLab), imefanikisha mafunzo ya Tehama na Coding kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 2000 nchini pamoja na kuwapa ushauri wa kitaaluma ili kuwajenga kimasomo vijana hao.

