×

Simba Yawasimamisha Clatous Chama na Nassoro Kapama

Klabu ya Simba Desemba 21, 2023 imewasimamisha wachezaji wake Clatous Chama na Nassoro Kapama kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao watapelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya klabu ili kujadiliwa nakujua hatima yao.

Klabu hiyo imewakumbusha watumishi wa klabu hiyo kufuata misingi ya maadili na nidhamu na kusema klabu haitasita kuwachukulia hatua watumishi watakaoonesha utovu wa nidhamu.

Leave a Comment