
Kampuni ya Puma Energy Tanzania imekabidhi mifuko 600 ya cement, Mabati 800 na Nondo 1000, vyote vikiwa na gharama isiyopungua TSH Milion 70.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Bi Fatma Mohemed Abdallah, Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited ndugu Godluck Shirima amesema;
“ Bodi ya wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake Dr. Selemani Majige, Menejimenti ya Kampuni chini ya uongozi wa Bi Fatma Mohamed Abdallah, wafanyakazi na wadau wote wa Puma Energy Tanzania Limited wameguswa na kuhuzunishwa sana na mafuriko yalio wakuta wenzetu wa Katesh na hivyo wakatuelekeza kuleta msaada huu wa vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi na jitiada za Serikali kuwajengea makazi waathirika waliopoteza makazi yao kwenye mafuriko.

Puma Energy pia ni Muathirika wa mafuriko haya, ambapo kituo chao cha Kateshi kiliharibiwa vibaya na mafuriko, kwa hiyo kama mhanga na mkazi wa Kateshi, kampuni iliona ni vyema kutoa mchango wake kwa jamii ya Katesh.
Kwa upande wake Mhe. Janeth Mayanja, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, akipokea na kushukuru msaada huo kutoka kampuni ya Puma Energy amesema, “ msaada huu wa vifaa vya ujenzi kutoka Puma Energy umekuja muda muafaka kwakuwa Serikali sasa ipo kwenye mkakaati wa kuanza kuwajengea wananchi waliopoteza makazi yao kwenye mafuriko.

Alisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi makini wa Dr. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuwajengea nyumba wananchi waliopoteza makazi na sasa wapo katika hatua za kupima viwanja, pia amewaomba wadau wengine kuiga mfano wa Puma Energy na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwasaidia waathirika wa mafuriko na hasa kwa kutoa vifaa vya ujenzi kwakua ndio vinavyo hitajika zaidi kwa sasa.
Kampuni ya Puma Energy iliwakilishwa na Bw. Godluck Shirima (Meneja Mahusiano), Bi. Lilian Kanora ( Meneja Masoko) na Bw. Joseph Jaruma ( Meneja Rasilimali Watu).