
Dar es Salaam 4 Januari 2024: Kampeni ya Magifti Dabo dabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo kwa kutumia huduma za kampuni hiyo imeendelea kuwanufaisha wananchi kwa kumwaga zawadi kibao kwa washindi wa kampeni hiyo.
Pamoja na kumwaga zawadi mbalimbali kwa washindi kama pesa taslimu shilingi milioni moja, milioni tano, seti ya vifaa vya ndani vya kisasa kutoka Kampuni ya Hisense ikijumuisha friji, microwave, seti ya muziki wa kisasa (sound bar) na runinga ya kisasa mwanadada Christina Latin Mrua mkazi wa Salasala jijini Dar amejishia vifaa hivyo na kukabidhiwa seti mbili za vifaa hivyo kwenye hafla iliyofanyika Salasala Mabanda Mengi.

Christina akiwa amejaa furaha alikabidhiwa vifaa hivyo seti mbili seti moja ni yake na nyingine mpendwa wake na Meneja Mauzo wa Tigo Kinondoni Kaskazini, Shadrack Mutalemwa na kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na umati wa mashuhuda.
Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo mshindi huyo aliongeza kwa furaha na kuipongeza kampuni ya Tigo kwa kumfanyia jambo ambalo hakulitegemea na kuwaomba watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao wa simu hiyo ili nao waweze kujishindia kama yeye.
Kwa upande wake Meneja Mutalemwa akikabidhi vifaa hivyo alimpongeza mshindi huyo kwa kutumia huduma za Tigo na kuwaomba watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao huo kwani kampeni hiyo bado inaendelea na zawadi bado ni nyingi na zawadi kubwa katika kampeni hiyo ni magari ya kisasa.
Mutalemwa amesema katika kampeni kama inavyoitwa Magifti Dabo dabo hivyo kila zawadi inayotolewa inatolewa Dabodabo iwe gari, vifaa vya nyumbani na hata pesa.
Alimalizia kwa kusema unachotakiwa ni kutumia tu huduma mbalimbali za kampuni hiyo kama vile kufanya miamala, kulipia huduma mbalimbali kama vile luku, kununua vocha kwa kutumia tigo pesa au za kukwangua, kuweka bando na huduma nyingine zote